Jeshi lafyatua risasi ndani ya kambi Ivory Coast

Haki miliki ya picha AFP / GETTY IMAGES
Image caption Jeshi lafytua risasi ndani ya kambi Ivory Coast

Kikosi maalum cha jeshi nchini Ivory Coast, kimefyatua risasi katika kambi za kijeshi nchini humo.

Hilo linatukia mwezi mmoja baada ya walinzi kadhaa ndani ya jeshi, kupanga uasi uliodumu masaa 48, kulalamikia hali mbovu katika kambi za kijeshi na mshahara duni.

Uasi katika mji Adiake ulioko kusini mashariki mwa nchi hiyo, karibu na mpaka na Ghana, pia ulisemekana kutokana na mishahara mibovu.

Mkazi mmoja mjini Adiake ameiambia BBC kuwa, milio ya kwanza ya risasi ilisikika mwendo wa saa moja asubuhi saa za huko.

Kila mtu alisalia nyumbani, huku biashara na shule zikifungwa.

Image caption Jeshi lafytua risasi ndani ya kambi Ivory Coast

Waasi wamo ndani ya jeshi maalum la Ivory Coast - kikosi maalum ambacho mara nyingi hakionekani hadharani, na kinachoaminika kuwa tiifu kwa serikali.

Kwa mjibu wa vyombo vya habari nchini humo, kamanda wao Jenerali Lassina Doumbia, amezuilia mafao ya kila siku kutokana na majukumu yao ya kulinda mpaka kati ya Ivory Coast na Ghana.

Hakuna taarifa zozote kutoka makao makuu ya jeshi au serikali.