Lwandamina-Tutawafunga Simba

Image caption Nembo ya Yanga

Kocha wa mabingwa soka Tanzania bara Timu ya Yanga Mzambia George Lwandamina ametamba kwamba mechi dhidi ya timu ya Ngaya Club ya Comoro katika mchezo wa klabu bingwa afrika zitawapa taswira nzuri kabla ya kuvaana na maasimu wao Timu ya Simba Februari 25, mwaka huu katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Yanga inatarajia kuchuana na Simba Februari 25, mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam .

Kwa sasa Yanga wapo kileleni mwa Ligi hiyo kwa alama 49, wakifuatiwa na Simba yenye alama 48 baada ya timu zote kucheza michezo 21.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi Januari 10, mwaka huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar na Simba ikashinda kwa penalty 4-2 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90