Kamanda wa polisi apigwa risasi Kenya

Kamanda alipigwa risasi wakati wa oparesheni dhidi ya wafugaji waliovamia mashamba ya kibinafsi
Image caption Kamanda alipigwa risasi wakati wa oparesheni dhidi ya wafugaji waliovamia mashamba ya kibinafsi

Kamanda mmoja wa polisi eneo la Laikipia ya kati nchini Kenya, amesafirishwa hadi mji mkuu Nairobi, kwa matibabu maalum baada ya kupigwa risasi wakati wa mapigano na wafugaji.

Gazeti la Nation la nchini Kenya lilisema kuwa Mbelengo Mohare, alikuwa akiongoza oparesheni dhidi ya wafugaji ambao walikuwa wamevamia mashamba ya kibinafsi miezi ya hivi majuzi.

Alipelekwa kupata matibabu hospitali iliyokuwa karibu kalba ya kusafirishwa hadi Nairobi.

Kamishina wa eneo hilo Onesmus Musyoki, anasema kuwa oparesheni hiyo bado inaendelea.

Image caption wavugaji