Kesi ya kupinga utawala wa Mugabe yatupwa na mahakama

Mugabe ana umri wa miaka 92 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mugabe ana umri wa miaka 92

Kesi iliyowasilishwa kwenye mahakama ya kikatiba nchini Zimbabwe na kiongozi wa maandamano Promise Mkwananzi, ya kupinga utawala wa Rais Robert Mugabe imetupilikwa mbali.

Kundi la Tajamuka lilitaka kuonyesha kuwa raia Mugabe mwenye umri wa miaka 92 hayuko katika hali nzuri kuongoza kutokana na umri wake.

Mahakama ilitulipia mbali kesi hiyo ikisema kuwa bwana Mkwananzi alishindwa kumkabidhi Mugabe makaratasi ya kesi.

Sasa Mkwananzi ana siku 30 za kuchukua hatua zinazohitajika kabla ya kupeleka tena kesi hiyo mahakamani.

Image caption Promise Mkwananzi