Familia yenye watu 500 yapiga picha China

Familia ya Ren yapiga picha kwa pamoja Haki miliki ya picha ZHANG LIANGZONG
Image caption Familia ya Ren yapiga picha kwa pamoja

Zaidi ya jamaa 500 wa familia moja huko China wamepiga picha ya familia.

Picha hizo zilichukuliwa wakati wa kusherehekea mwaka mpya nchini humo ambao huadhimishwa na familia kubwa na vyakula.

Mpiga picha Zhang Liangzong alipiga picha hizo kwa kutumia ndege isiokuwa na rubani karibu na eneo la kitalii la Shishe.

Aliambia BBC kwamba familia ya Ren ambayo inatoka kijijini inadaiwa kuanza miaka 851 iliopita lakini rekodi ya udugu wao haijaangaziwa kwa zaidi ya miongo minane.

Wazee wa kijiji hivi majuzi walianza kuangazia rekodi za familia hiyo na kufanikiwa kupata ndugu wengine 2000 kupitia vizazi saba, alisema Bw Zhan.

Waliadhimisha mafanikio hayo kwa kuweka mkutano mkubwa na kuweza kupata zaidi ya wanachama 500 wa familia hiyo.

Haki miliki ya picha ZHANG LIANGZONG
Image caption Familia ya Ren katika picha iliopigwa katika eneo moja la kitalii

Chifu wa kijiji hicho Ren Tuanjie ameambia chombo cha habari cha Xhinua :Sababu moja ni kuelewa kule wajukuu wetu wameenea ,kule ambako walikuwa na kule walikoishi ili kuwajua mababu zao.

Na sababu nyengine ilikuwa kuwataka wajukuu wetu kujua mizizi yao ,ili popote wendapo wasisahau kule watokako ,alisema bw Ren, ambaye antoka katika kizazi cha 26 na mabye jina lake linamaanisha kukutana upya nchini China.

Waliadhimisha mafanikio hayo kwa kuweka mkutano mkubwa na kuweza kupata zaidi ya wanachama 500 wa familia hiyo.