Qatar inatumia dola milioni 500 kwa wiki kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2022

Ujenzi wa uwanja nchini Qatar Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ujenzi wa uwanja nchini Qatar

Qatar inatumia karibu dola milioni 500 kwa wiki kwa miradi mikubwa wakati inajiandaa kwa Kombe la Dunia la mwaka 2022, waziri wake wa fedha amesema.

Ali al-Emadi anatarajia matumizi hayo ya fedha kuendelea kwa kipindi cha miaka mitatu au minne inayokuja kwa kujenga viwanja vipya, barabara, reli na hospitali.

Zaidi ya dola bilioni 200 zitatumiwa kwa jumla, na taifa hilo lenye utajiri wa mafuta.

Lakini bwana Emadi amekana kuwa mipango hiyo huenda ikisababisha kinyanganyiro hicho cha mwaka 2022 kuwa ghali zaidi duniani.

Kombe la dunia la mwaka 2014 lililoandaliwa nchini Brazil, liliripotiwa kugharimu dola bilioni 11 kuandaliwa, huku nayo Urusi ikiongeza bajeti ya kuandaa kombe la mwaka 2018 hadi dola bilioni 10.7.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ali al-Emadi anasema pesa hizo zimetokana na kupunguzwa bajeti

Wanakandarasi nchini Qatar, wamewaleta maelfu ya wafanyakazi wahamiajia hasa kutoka mataifa ya kusini mwa Asia, ambao wapiganiaji wa haki za binadamu wanasema kuwa wanalazimishwa kufanya kazi katika mazingira mabaya.

Serikaloi ya Qatar imekana haya na mwezi Disemba ilifanya mabadiliko yenye lengo la kuboresha haki za wafanyakazi wahamiaji.