Je, Mohamed Farmajo ni nani?

Bendera ya Somalia
Image caption Bendera ya Somalia

Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo alizaliwa 1962 mjini Mogadishu kutoka katika familia ya Gedo kusini magharibi mwa Somalia.

Mwaka 1985 alichaguliwa kuwa katibu wa kwanza katika ubalozi wa Washington DC.

Mwaka 1989, aliondoka na kujipatia shahada yake ya historia katika chuo kikuu cha Buffalo mjini New York .

Wakati huo Farmajo alitafuta hifadhi ya kisiasa nchini Marekani baada ya serikali ya Somalia kuanguka 1991.

Aliendelea na masomo yake katika chuo kikuu cha Buffalo na kujipatia shahada ya uzamili katika somo la sayansi ya siasa pamoja na mahusiano ya kimataifa.

Rais Sharif Ahmed wa Somalia alimchagua Farmajo kuwa waziri mkuu mnamo mwezi Oktoba 2010 ili kumrithi Omar Abdirashid Sharmake ambaye alijiuzulu katika wadhfa wake kufuatia mgogoro.

Farmajo alijiuzulu katika wadhfa wake mnamo mwezi Juni 2011 baada ya shinikizo ya jamii ya kimataifa miongoni mwa makubaliano ya Kampala kati ya rais Ahmed na spika wa bunge Aadan ambapo makubaliano ya kamati hiyo ya mpito yaliongezwa hadi mwezi Agosti 2012.

2011 Farmajo alianzisha chama kipya cha Somali Justice and Equality kwa jina maarufu Tayo.

Farmajo ni katibu mkuu wa Tayo ambacho kinaongozwa na mwenyekiti Mariam Qasim,aliyekuwa waziri wa maswala ya wanawake.

Tayo ni chama cha kwanza cha kisiasa nchini Somalia kinachoongozwa na mwanamke.

Farmajo anazungumza lugha ya Kisomalia na Kiingereza na ana uraia wa Somalia na Marekani.

Mwaka 2012 Mohamed alikuwa mgombea wa urais katika uchaguzi huo ambapo aliangushwa katika raundi ya kwanza ya uchaguzi huo.