Sweden yafanyia majaribio saa za kufanya kazi

Emilie Telander (kulia) anasema ana uchovu mwingi kwa vile amerejea muda wa kawaida wa kufanya kazi
Image caption Emilie Telander (kulia) anasema ana uchovu mwingi kwa vile amerejea muda wa kawaida wa kufanya kazi

Sweden imekuwa ikifanyia majaribio muda wa masaa sita, huku wafanyakazi wakipata saa chache za kufanya kazi, sasa majaribio hayo ya miaka miwili yamekamilika na yote yanaonekana kuenda salama

Muuguzi kwenye makao ya watu wazee Emilie Telander, mwenye umri wa miaka 26 anasema hajafurahia kuona muda huo ukifika kikomo, tena ameambiwa kufanya kazi tena muda wa masaa nane.

"Ninahisi kuwa mchovu zaidi kuliko nivyokuwa awali, anasema kuwa sasa ana muda mfupi nyumbani kupika na kusoma na bintiye mwenye umri wa miaka minne.

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Gothenburg umekuwa ukifanyia majaribio muda wa kufanya kazi wa saa nane

Wakati wa kipindi cha majaribio, wafanyakazi wote walikuwa na nguvu. Niliweza kuona kuwa kila mtu alikuwa na raha.

Bi Telander alikuwa kati ya wauguzi 70 ambao masaa yao yalikuwa yamepungua wakati wa majaribio hayo.

Baada ya kubuniwa kuboresha sekta ambayo ina changamoto za kupata wafanyakazi wa kutosha kuwaangalia watu wazee nchini humo, wauguzi zaidi waliajiriwa ili kusaidia muda uliopunguzwa.

Image caption Makao ya watu wazee ya Svartedalen

Watafiti huru nao walilipwa kuwasoma wafanyakazi ambao waliiendelea kufanya kazi muda wa kawaida.

Ripoti ya mwisho inaratajiwa kutolewa mwezi ujao, lakini takwimu zilizotolewa zinaunga mkono maoni yake Telander.

Wakati wa miezi 18 ya majaribio wauguzi ambao walifanya kazi saa chache waliomba likizo chache, na walifanya kazi kwa asilimia 85 zaidi kama vile kuwatembeza wagonjwa na kuimba nao.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Huenda muda wa kawaida wa saa nane wa kufanya kazi ukasalia

Hata hivyo mradi huo ulipata kukosolewa na wale waliokuwa na wasi wasi kuwa gharama yake ilikuwa ya juu kuliko manufaa.

Wapinzani wa kati-kulia, walipeleka mswada wakati manispaa ya Gothenburg wakitaka kuusitisha mradi huo mapema mwezi wa tano, wakidai kuwa haikuwa vyema kuwekeza pesa za walipa kodi katika mradi ambao haukuwa na manufaa ya kiuchumi.

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Utafiti zaidi unafanyiwa mfumo wa kupokezana kazi nchini Sweden