Serikali Guinea Ikweta yahamisha makao yake makuu

Guinea Ikweta
Image caption Guinea Ikweta

Serikali ya Guinea ya Ikweta imehamisha Makao yake makuu kutoka katika mji ulioko pwani wa Malabo kwenda katika mji ulioko kwenye ukanda wa msitu wa mvua.

Rais Teodoro Obiang Nguema amechagua eneo jipya la Djibloho kama moja ya miji anayotaka kuiendeleza kwa kutumia utajiri wa mafuta wa nchi hiyo.

Mji huo uko karibu na mbuga nyingi za taifa za nchi hiyo.

Habari zinasema wabunge wataanza kukaa huko kwa miezi mitatu. Waziri mkuu Francisco Pascual Obama Asue amewaonya wabunge hao wasitumie muda wa kukaa huko kama wako mapumziko.