Arsene Wenger: Tuna matumaini kushinda ligi Uingereza

Wenger asema hajavunja tamaa ya kushinda ligi ya EPL Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wenger asema hajavunja tamaa ya kushinda ligi ya EPL

Arsenal ni sharti iamini kwamba bado inaweza kushinda ligi ya Uingereza msimu huu licha ya pengo la pointi 12 kati yake na viongozi wa ligi Chelsea ,kulingana na mkufunzi Arsene Wenger.

The Gunners, ambao kwa mara ya mwisho walishinda ligi mwaka 2004 walishuka hadi nafasi ya 4 baada ya kushindwa 3-1 na Chelsea Jumamosi iliopita.

Kikosi cha Wenger kinaialika Hull City katika uwanja wa Emirates baada ya kupoteza mechi nne kati ya tisa ilizocheza.

''Bado hatujasalimu amri'', alisema raia huyo wa Ufaransa.''Hata iwapo unadhani tumeshafanya hivyo, mimi bado sijasalimu amri-hatuweza kufikiria hivyo''.

Kwa sasa ni pointi tano pekee zinazotenganisha Tottenham ilio nafasi ya pili na Manchester United iliopo katika nafasi ya sita.

Aliongezea Wenger: Tuko katika eneo ambalo ni gumu sana na ugombeaji wa kila nafasi ni muhimu sana msimu huu ikilinganishwa na ule uliopita.