Maandamano ya tamasha la muziki 'Sauti za busara' yafanyika TZ

Mwaka huu tamasha litakuwa na wasanii wa muziki wapatao 400 kutoka kila kona ya bara la Afrika.
Image caption Mwaka huu tamasha litakuwa na wasanii wa muziki wapatao 400 kutoka kila kona ya bara la Afrika.

Maandamano ya uzinduzi wa tamasha kubwa la muziki Afrika Mashariki Sauti za Busara yemefanyika.

Maandamano haya ni ya umbali wa kilometa mbili kutoka Mnara wa Kisonge hadi Forodhani.

Image caption Baadhi ya raia waliohudhuria maandamano hayo

Mwaka huu tamasha litakuwa na wasanii wa muziki wapatao 400 kutoka kila kona ya bara la Afrika.

Kauli mbiu ya tamasha hili ni 'Umoja wa Afrika'.

Waandaaji wa tamasha hili wanasema muziki una nguvu ya kuwaunganisha watu kutoka tofauti zozote zile.

Image caption Baadhi ya wasanii walioshiriki katika tamasha hilo

Katika siku hizi tatu za tamasha Zanzibar inatarajia kunufaika sana kiutalii na kibiashara kwa ujumla kutokana na kuwepo kwa wageni wengi .

Kwa mujibu wa baadhi ya makisio, tangu kuanzishwa kwa Tamasha hili mwaka 2004, tamasha hili limeiingizia Zanzibar takribani Dola Milioni 70 za mapato.

Image caption Wasanii wakionyesha baadhi ya michezo yao

Kati ya wasanii wakubwa wanaotarajiwa hapa ni Mmoroko Mehdi Nassouli anayejulikana na 'Bob Maghrib', wakati Mzanzibari Mohammad Issa Matona akitarajia kuchagiza tamasha hilo la muziki wake wa miondoko ya Taarab.