Ujerumani kuwatimua watafuta hifadhi zaidi

Kusafirishwa kwa watafuta hifadhi kuenda nchini Afghanistan kumepingwa vikali Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kusafirishwa kwa watafuta hifadhi kuenda nchini Afghanistan kumepingwa vikali

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajiwa kuanzisha mpango mpya ya kuongeza idadi ya watafuta hifadhi wanaosafirishwa kutoka nchini humo wakirudishwa makwao.

Hatua hizo ni pamoja na kuzifanyia uchunguzi simu za watafuta hifadhi ili kuwatambua na kuongeza fedha zinazolipwa kwa wale ambao wanakubali kurudi makwao kwa hiari.

Suala la uhamiaji limekumbwa na siasia nyingi nchini Ujerumani kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu.

Mtafuta hifadhi mmoja aliwaua watu 12 kwenye soko la Krislamia mjini Berlin mwezi Disemba.,

Chansela Merkel anakutana na viongzoi wa majimbo, kujadili mipango mipya ya kuharakisha kusafirishwa kwa watafuta hifadhi hao.

Vituo vitawekwa karibu na viwanja vya ndege kuwazuiliia watafuta hifadhi waliokataliwa makwao siku au wiki kadha kabla ya kusafirishwa tena.

Serikali ina mipango ya kutumia Euro milioni 90 mwaka huu kwa mpango huo. Pesa zaidi zitatolewa kwa wale watakoamua kurudi kwa haraka.

Karibu watafuta hifadhi 890,000 waliwasili nchini Ujerumani mwaka 2015.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Angela Merkel alipata umaarufu nyumbani na ng'ambo kwa kuwaruhusu watafuta hifadhi wengi kuingia Ujerumani