Adama Barrow asema Gambia itasalia ndani ya ICC

Bw Barrow alimshinda vibaya Bw Jammeh katika uchaguzi mkuu Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bw Barrow alimshinda vibaya Bw Jammeh katika uchaguzi mkuu

Rais mpya wa Gambia Adama Barrow amerejelea ahadi yake aliyotoa wakati wa uchaguzi mkuu, kwamba taifa hilo halitajiondoa kutoka ndani ya mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, (ICC), na kubadili uamuzi wa mtangulizi wake Yahya Jammeh, ambaye alikuwa anapinga mahakama hiyo, huku akiitaja kama "Mahakama ya kimataifa inayoendesha hukumu zake kwa misingi ya ubaguzi wa rangi, hasa ikiwahukumu tu waafrika".

Bw Barrow alisema hayo, baada ya kukutana kamishena wa tume ya ushiriikiano na maendeleo ya jumuia ya mataifa ya bara Ulaya, Neven Mimica, katika mji mkuu, Banjul.

Bw Mimica, alisifia tangazo hilo kwa kuandika kwwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter:

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Ujumbe wa Neven Mimica katika Twitter

Bw Barrow alishinda uchaguzi mkuu wa Disemba 1, 2016, kwa ahadi ya kupigania haki za binadamu na uhuru, na kumaliza unyanyasaji ambao raia wa Gambia wamepitia wakati wa utawala wa miaka 22 wa Bw Jammeh.

Naye mwaandishi mmoja wa habari wa Uingereza nchini Gambia, ameandika katika mtandao wake wa Twitter kuwa Jumuia ya bara Ulaya, imeahidi kuzidisha mara dufu msaada wake kwa taifa hilo dogo la Afrika Magharibi:

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Ni twitter ya Ruth Maclean