Mauaji na magari mengi yaibwa baada ya polisi kugoma Brazil

Mauaji yaongezeka na magari mengi kuibwa baada ya polisi kugoma Brazil Haki miliki ya picha AP
Image caption Mauaji yaongezeka na magari mengi kuibwa baada ya polisi kugoma Brazil

Brazil, Argentina zashinda Idadi ya watu waliouawa nje na ndani ya mji wa Victoria nchini Brazil tangu polisi waanze mgomo siku ya Jumamosi, imeongezeka hadi watu 95.

Wanajeshi zaidi wametumwa lakini wenyeji wameutaja mji huo kuwa ulio na vurugu, huku shule na maduka yakisalia yamefungwa.

Siku ya Jumatano magari 200 yaliripotiwa kuibwa. Polisi wanataka kulipwa mishahara ya juu na marupurupu zaidi.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mauaji yaongezeka na magari mengi kuibwa baada ya polisi kugoma Brazil

Polisi wanadai kuwa mishaharaya dola 830 kila mwezi ni ya chini.

Lakini serikali inasema kuwa haina uwezo wa kulipa marupurupu hayo. Kiongozi wa chama anasema kuwa wenyeji hawastahili kuwalaumu polisi kwa kugoma, bali serikali kwa kukosa kulipa suala la usalama wa taifa kipaumbele