Nyangumi 400 wakwama kwenye ufukweni New Zealand

Huwezi kusikiliza tena
Mamia wajitokeza kuwaokoa nyangumi waliokwama New Zealand

Watu wa kujitolea wanasaidia katika juhudi za kuwaokoa nyangumi karibu 100 waliokwama kwenye ufuo wa bahari.

Nyangumi hao ni sehemu ya nyangumi 400 waliokwama baharini usiku wa kuamkia leo.

Takriban nyangumi 300 walifariki usiku katika ufukwe wa Farewell Spit, katika kisiwa cha Kusini, katika kisa ambacho kinatajwa kuwa kibaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.

Mamia ya raia wa kujitolea wakisaidiana na maafisa wa uhifadhi wa wanyama na mazingira wanafanya juhudi za kusaidia kuwarejesha nyangumi hao baharini.

Nyoka apatikana kwenye ndege ya Emirates

Mwanamke ajuta kumtia nyoka katika ndewe yake

Wamekusanyika kwenye foleni kubwa kujaribu kuwaokoa nyangumi hao.

Wanasayansi kufikia sasa bado hawajafanikiwa kufahamu ni kwa nini nyangumi hufika kwenye ufuo wa bahari.

Lakini wakati mwingine inadhaniwa huwa inatokea kwa sababu nyangumi ni wazee sana au wanaugua, au wameumia, au wamepoteza mwelekeo hasa maeneo ambayo ufuo si laini.

Wakati mwingine, nyangumi anapokwama baharini, atawalilia wenzake ambao watafika kujaribu kumuokoa. Wengi mara nyingi nao hukwama maji yanapokupwa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watu wa kujitolea wanajaribu kuwarejesha nyangumi hao baharini

Idara ya uhifadhi baharini imesema ilipokea taarifa kwamba huenda kuna nyangumi waliokuwa wamekwama Alhamisi usiku.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kisa cha sasa ndicho kibaya zaidi kutokea nchini humo

Hata hivyo, hawakuanzisha operesheni ya kujaribu kuokoa nyangumi hao kwa sababu ilikuwa hatari sana kujaribu kufanya operesheni hiyo gizani, gazeti la New Zealand wameripoti.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mara kwa mara nyangumi hukwama Farewell Spit

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii