Bidhaa za kutengeneza vidonge vya kusisimua mwili vyakamatwa Uholanzi

Uholanzi inafahamika kama mtengenezaji mkubwa wa vidonge vya kusisimua mwili duniani. Haki miliki ya picha DEA
Image caption Uholanzi inafahamika kama mtengenezaji mkubwa wa vidonge vya kusisimua mwili duniani.

Polisi nchini Uholanzi wanasema kuwa wamekamata bidhaa ambavyo vingetumiwa kutengeneza vidonge bilioni moja vya kusisimua mwili.

Bidhha hizo zilikuwa ndani ya lori moja lililokuwa limeegeshwa katika kijiji cha Rilland karibu na mpaka wa Ubelgiji.

Bidhaa hizo ni pamoja na chupa 100,000 za gesi ya Hydrogen, kilo 15,000 za Caustic Soda na lita 3000 ya kemikali zingine.

Polisi hawakutoa makadirio ya tamani ya bidhaa hizo na pia hawakusema ikiwa kuna mtu alikamatwa.

Walisema kuwa wanachunguza ni nani anamiliki bidhaa hizo.

Uholanzi inafahamika kama mmoja ya watengenezaji wakubwa wa vidonge vya kusisimua mwili duniani.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii