Uingereza kuajiri vijana 5000 kulinda mtandao

Serikali inasema usalama katika mitandao ni sekta inayokuwa haraka, na watu elfu sitini wanafanya kazi katika sekta hiyo.
Image caption Serikali inasema usalama katika mitandao ni sekta inayokuwa haraka, na watu elfu sitini wanafanya kazi katika sekta hiyo.

Serikali ya Uingereza inasema kuwa inataka kuanzisha kizazi kipya cha wataalmu wa usalama katika mitandao ya kompyuta, kupambana na kile kinachoona ni tishio kubwa kwa nchi.

Inataraji kuajiri watoto wa shule matineja zaidi ya elfu tano, ambao wako tayari kufunzwa kwa saa nne kila juma.

Mradi huo wa miaka mitano, utakaogharimu dola milioni 25, utaingizwa katika mitaala ya kawaida ya shule.

Masomo ya chuo kikuu yatagharimiwa na serikali, na wale waliofuzu watapatiwa kazi.

Serikali inasema usalama katika mitandao ni sekta inayokuwa haraka, na watu elfu sitini wanafanya kazi katika sekta hiyo.