Watu wengi wahamishwa wakati wa kuteguliwa bomu Ugiriki

Bomu hilo huenda ni kutoka vita kuu vya pili vya Dunia Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bomu hilo huenda ni kutoka vita kuu vya pili vya Dunia

Zaidi ya watu elfu 70 wanahamishwa kwa mda huko mjini Thessaloniki nchini Ugiriki, ili kutoa nafasi ya kuteguliwa bomu moja la zamani ambalo ni mabaki ya zana za vita za tangu enzi ya vita kuu vya pili vya dunia.

Bomu hilo ambalo lina uzito wa zaidi ya robo tani lilipatikana wakati wa ujenzi wa kituo kimoja cha kuuza mafuta .

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bomu hilo liligunduliwa karibu na kituo cha mafuta wiki iliyopita

Sasa Kila mmoja aliye eneo la kilomita mbili mraba inabidi ahamishwe kwa lengo la kufanikisha uteguzi salama wa bomu hilo.

Haijabainika kama lilikuwa la upande wa majeshi ya muungano au upande wa wajerumani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bomu hilo liligunduliwa karibu na kituo cha mafuta wiki iliyopita