Raia waitaka serikali ijiuzulu Romania

Romania
Image caption Raia wa Roamnia wakiwa kwenye maandamano

Maelfu ya waandamanaji kwa mara nyingine wameingia barabarani nchini Romania, huku wakitaka serikali ijiuzulu.

Idadi kubwa ya waandamanaji iko katika uwanja wa ushindi maarufu kama Victory Square katikati mwa mji mkuu wa Bucharest, ambapo waandamanaji wamejipanga katika mistari ya rangi ya blu, manjano na nyekundi zikiashiria rangi ya bendera ya nchi hiyo.

Maandamano yanapinga kauli iliyotolewa na waziri wa mambo ya nje baada ya kusema kwamba serikali yake haiwezi kujiuzulu mpaka itakapopigiwa kura ya kutokea na imani bungeni.

Maandamano ya wiki mbili yamelazimisha serikali kufuta kauli yake ambayo ingepunguza nguvu ya waendesha mashtaka dhidi ya kesi za dawa za kulevya, na pia kusababisha waziri wa sheria kujiuzulu.