Maandamano ya 'umoja' Mexico kumpinga Donald Trump

Kinyago cha Donald Trump 12 Februari 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waandamanaji wamewataka raia wa Mexico kuungana dhidi ya Trump

Maelfu ya watu wameandamana nchini Mexico kupinga sera za uhamiaji za rais wa Marekani Donald Trump pamoja na mpango wake wa kujenga ukuta katika mpaka wa mataifa hayo mawili.

Waandamanaji katika zaidi ya miji kumi Mexico, waliandamana barabarani wakiwa wamevalia mavazi meupe na kupeperusha bendera za Mexico na kubeba mabango ya kumshutumu Trump.

Waandalizi wanasema walitaka kutuma ujumbe kwamba Mexico imeungana dhidi ya Trump.

Pia walimshutumu Rais Enrique Pena Nieto kwa kutokabiliana vilivyo na rushwa na ongezeko la uhalifu wa kutumia mabavu.

Mmoja wa waandamanaji Maria Amparo Cassar amesema sera za uhamiaji za Trump ni "tishio kwa jamii ya kimataifa."

"Isisahaulike kwamba jamii ya Marekani iliundwa na wahamiaji na inaendelea kuundwa na wahamiaji," amesema.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Raia wa Mexico wanatazama sera za uhamiaji za Trump kuwa zisizo za haki

Waandamanji katika mji mkuu, Jiji la Mexico, walibeba mabango ya kuonyesha umoja.

Moja lilikuwa na ujumbe: "Gracias, (Asante) Trump, kwa kuunganisha Mexico!"

Bw Trump anapanga kujenga ukuta mpaka wa Marekani na Mexico na amekuwa akisisitiza kwamba raia wa Mexico ndio watalipia ujenzi huo.

Hilo limewakera taia wa Mexico na rais Pena Nieto mara kwa mara amesisitiza kwamba taifa lake halitalipia ukuta huo.

Majuzi, mkutano uliopangwa kati ya wawili hao ulitibuka.


Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maelfu ya watu waliandamana Mexico City, na hapa wanaonekana Plaza Angel Independencia
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Waandamanji wamesema wanataka kuonesha wameungana dhidi ya Trump

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii