Mizoga ya nyangumi 300 kuhamishwa New Zealand

Nyangumi Golden Bay, 10 Februari 2017. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nyangumi waliofariki waliwekwa alama ya mkasi "X"

Maafisa wa serikali nchini New Zealand wamesema watahamisha mizoga ya mamia ya nyangumi waliofariki baada ya kukwama kwenye ufukwe wa bahari.

Mizoga hiyo ya nyangumi zaidi ya 300 itahamishwa kwa kutumia matrekta makubwa ya na kuzikwa kwenye vichungu vya mchanga kwenye ufukwe mbali na eneo ambalo hutembelewa na watu Farewell Spit, katika Kisiwa cha Kusini.

Maafisa wa uhifadhi Jumatatu walifika na kutoboa machimo kwenye mizoga hiyo ili kuachilia gesi inayozalishwa miili hiyo inapoanza kuoza.

Kumekuwa na wasiwasi kwamba mizoga hiyo huenda ikaanza kupasuka na kulipuka.

Kisa cha Alhamisi, ambapo zaidi ya nyangumi 400 walikwama ufuoni ndicho kibaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.

Nyangumi 300 kati yao walifariki lakini waliosalia walisaidiwa kurejea baharini.

Haijabainika ni nini kiliwafanya nyangumi hao kukwama baharini siku hiyo.

Wengine karibu 200 walifika na kukwama kwenye bahari tena Jumamosi.

Nyangumi waliokwama Jumamosi walisaidiwa kurejea baharini ingawa maafisa wa uhifadhi wanasema nyangumi hao wamo karibu na ufukwe na kuna hofu huenda wakakwama tena.

Kwa sasa kuna boti lililo na wafanyakazi wa uhifadhi ambao wameachwa eneo hilo kushughulikia dharura yoyote itakapotokea.

limeachwa eneo hilo kuwasahicho cha kukwama conservation workers pierced the bodies to release gas built up during decomposition, following warnings the carcasses might explode.

Image caption Mizoga hiyo itapelekwa eneo ambalo watu hawafiki kwa wingi ufukweni Farewell Spit
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu wa kujitolea wamekuwa wakijipanga kwenye foleni baharini kuzuia nyangumi hao kurejea tena ufukweni

Mbona nyangumi hufika ufukweni?

Wanasayansi kufikia sasa bado hawajafanikiwa kufahamu ni kwa nini nyangumi hufika kwenye ufuo wa bahari.

Lakini wakati mwingine inadhaniwa huwa inatokea kwa sababu nyangumi ni wazee sana au wanaugua, au wameumia, au wamepoteza mwelekeo hasa maeneo ambayo ufuo si laini.

Wakati mwingine, nyangumi anapokwama baharini, atawalilia wenzake ambao watafika kujaribu kumuokoa. Wengi mara nyingi nao hukwama maji yanapokupwa.

Baadhi ya nyangumi wataalamu wanadhania kwamba huenda nyangumi hao huwa wamekimbizwa na papa, kwani majeraha yaliyotokana na kuumwa na papa yamepatikana kwenye mizoga ya baadhi ya nyangumi waliofariki.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu wengi walijitolea kuwasaidia nyangumi hao kurejea baharini
Huwezi kusikiliza tena
Mamia wajitokeza kuwaokoa nyangumi waliokwama New Zealand

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii