Kanisa takatifu la 'mwujiza wa Yesu' lafunguliwa Israel

Lilichomwa na Wayahudi wenye itikadi kali Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kanisa takatifu la Galilee ambapo Yesu Kristu aliwalisha watu 5000 kwa mikate mitano na samaki wawili

Misa maalum imefanyika kufungua rasmi kanisa Katoliki Kaskazini mwa Israel ambalo liliteketezwa na Wayahudi wenye itikadi kali mwaka wa 2015.

Kanisa hilo lililoko eneo la Tabgha kando mwa ziwa la Galilee linaaminika na Wakristo kama eneo takatifu ambapo Yesu Kristo alifanya muujiza wa kuwalisha watu 5000 kwa mikate mitano na samaki wawili pekee.

Ukarabati wa kanisa hilo ulichukua miezi minane na kugharimu kima cha dola milioni moja.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kanisa hilo huwavutia mahujaji wengi Wakristo kila mwaka

Licha ya Wayahudi watatu wenye itikadi kali kupatikana na makosa ya kuchoma kanisa hilo hata hivyo hawakuhukumiwa.

Uvamizi huo uliharibu maktaba ya kanisa na jengo nzima.

Hata hivyo sakafu yake iliyotengenezwa karne ya tano ilinusurika uharibifu huo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kanisa hilo lilifunguliwa rasmi kwa misa Jumapili
Haki miliki ya picha AP
Image caption Ujumbe ulioandikwa kwa Kiebrania wa kulaani kuabudiwa kwa sanamu ulipatikana ukiwa umeandikwa kwa rangi nyekundu ukutani baada ya shambulio
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Shambulio hilo lilitajwa kama tukio la chuki dhidi ya Wakristo
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Inadaiwa kwamba serikali ya Israeli ilitumia karibu $400,000 kugharimia ukarabati wa kanisa hilo

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii