Nathan Dyer majeruhi nje kwa muda

ukaya
Image caption Nathan Dyer , aliyeshikiliwa kutokana na maumivu

Winga wa klabu ya Swansea Nathan Dyer atakua nje ya uwanja mpaka mwisho wa msimu wa ligi kuu nchini England

Winga huyo aliumia mshipa wa kifundo cha mguu katika mchezo wa ligi dhidi ya Leicester City siku ya jumapili .

Nyota huyu raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 29 amecheza michezo mitano toka Paul Clement ateuliwe kuwa meneja wa Swansea mwezi uliopita .

Swansea wataendelea kuikosa huduma ya winga mwingine machachari Jefferson Montero anyesumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.