Donald Trump asema Korea Kaskazini ni tatizo kubwa mno

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un

Rais wa Marekani Donald Trump ameizungumzia Korea ya Kaskazini baada ya kitendo chake cha hivi karibuni cha kurusha kombora lenye uwezo wa kubeba silaha za kinyuklia kwamba nchi hiyo ni tatizo kubwa mno.

Trump alitoa matamshi hayo alipokuwa akizungumza na waandishi habari akiwa pamoja na waziri mkuu wa nchi ya Canada, Justin Trudeau katika ikulu ya Marekani, Trump amesema kwamba ataishughulikia na nchi ya akizungumza kwa msisitizo juu ya kauli hiyo.

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa lina nia ya kufanya mkutano wa dharula muda mfupi ujao ili pamoja na mambo mengine kujadili juu ya kitendo cha Korea ya Kaskazini.

China imetoa angalizo kuwa kitendo hicho kimeiwekea msuguano wa kikanda na kutoa wito kwa pande zote kujiepusha na hatua yoyote ile ya uchochezi.

Naye msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Geng Shuang amesema kwamba Beijing ililipinga jaribio hilo, inagawa Pyongyang ilikuwa inaendelea na mipango yake ya uendelezaji silaha kutokana na mvutano ulioko baina ya Washington na Seoul