Kijana aponzwa na Adolf Hitler nchini Austria

Harald Hitler Haki miliki ya picha Heute.at
Image caption Kijana huyo alionekana akipigwa picha nje ya jumba alimozaliwa Hitler la Braunau am Inn

Polisi nchini Australia wametangaza kwamba imemkamata kijana mwenye umri wa miaka 25, ambaye alivalia mavazi yanayofanana na aliyewahi kuwa matawala wa manazi Adolf Hitler kwa makosa ya kuutukuza utawala na enzi ya wanazi na kusema kwamba kwa muujibu wa sheria kitendo hicho ni uhalifu nchini Austria.

Kijana huyo amekuwa akijiita Harald Hitler.

Polisi wamesema mwanamume huyo, ambaye ana masharubu yenye kushabihiana na dikteta Hitler, alionekana akijipiga picha nje ya nyumba alimozaliwa dikteta huyo mjini Braunau.

Inaelezwa kuwa kijana huyo alionekana pia katika miji ya Vienna na Graz.

Msemaji wa jeshi la polisi nchini Austria amesema kwamba vitendo vya kijana huyo havikuwa vya masihara hata kidogo ama sanaa ya maonesho, anajua fika alichokuwa akikifanya.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii