Ukame waangamiza mifugo Morogoro
Huwezi kusikiliza tena

Ukame waangamiza mifugo Morogoro, Tanzania

Baadhi ya wafugaji nchini Tanzania hasa kutoka mkoa wa Morogoro wamelazimika kuuza mifugo yao kwa bei ya kutupa huku wengine wakiachwa kufa bila usaidizi.

Hii inatokana na hali ya kiangazi inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini. Hata hivyo, mamlaka ya Mkoa imesema ina mpango wa kuweka miondombinu ya kudumu ili kupunguza tatizo hilo kwa siku zijazo.

Mwandishi wa BBC Aboubakar Famau alitembelea eneo hilo.

Mada zinazohusiana