UEFA: Barcelona wachapwa 4-0 ugenini kwa PSG

Barcelon Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Angel di Maria

Miamba wa soka wa Uhispania FC Barcelona wameanza vibaya hatua ya kumi na sita bora katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-0 ugenini dhidi ya Paris Saint Germain ya Ufaransa.

Angel di Maria alianza kuwaandikishia PSG goli kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja hadi wavuni na katika dakika ya 40 mshambuliaji mpya wa Wafaransa hao Julian Draxler akaongeza bao la pili.

Dakika ya 55 Angel di Maria tena akawachapa Barca bao la tatu, kabla ya Edinson Cavani kuhitmisha shughuli kwa bao la nne .

Katika mchezo mwingine Benfica ya Ureno wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Borrrusia Dotmund ya Ujerumani kwa bao la Konstantinos Mitroglo.

Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa michezo miwili Bayern Munich wakiwaalika Arsenal nao Real Madrid wakiwa wenyeji wa Napoli.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii