Michezo 16 ya Europa ligi inapigwa leo

Ulaya Haki miliki ya picha Google
Image caption Europa league

Michuano ya Europa ligi hatua ya 32 bora itachezwa leo kwa jumla ya nyasi za viwanja 16 kuwaka moto leo.

Manchester United wako kwao Old Trafford kucheza na St-Etienne ya France, Tottenham Hotspur watakua ugenini kucheza KAA Gent.

Waholanzi wa AZ Alkmaar tawakaribisha Lyon toka Ufaransa, Celta Vigo watakipiga na Shakhtar Donetsk, huku Borussia Monchengladbach wakicheza ugenini na Fiorentina.

Ludogorets wao watakipiga na FC Copenhagen, huku Athletic Bilbao wakipimana ubavu na Apoel Nicosia, Legia Warsaw watakua wenyeji Ajax , Anderlecht watakua nyumbani Ubeligiji kucheza na Zenit St Petersburg.

Villarreal watakua wenyeji wa Roma, Nao Hapoel Beer Sheva watachuana na Besiktas huku Paok wakiwa na shughuli pevu dhidi ya Schalke