Rais mpya wa Somalia Mohamed Farmajo akabidhiwa mamlaka

Rais mpya wa Somalia Mohamed Farmajo akabidhiwa mamlaka
Image caption Rais mpya wa Somalia Mohamed Farmajo akabidhiwa mamlaka

Aliyekuwa rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amemkabidhi mamlaka rais mpya aliyechaguliwa Mohamed Abdullahi Farmajo.

Rais huyo mpya alichaguliwa chini ya usalama mkali uliowekwa katika uwanja wa ndege uliopo mji mkuu wa Mogadishu kutokana na hofu ya shambulio la al-Shabab.

Farmajo alimshinda Mohamed ambaye alitaraji kwamba wabunge wangemchagua kwa awamu ya pili.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Rais Farmajo akabidhiwa mamlaka nchini Somalia

Mwandishi wa BBC Ibrahim Aden ametuma picha za aliyekuwa rais wa taifa hilo akimuonyesha mshindi wa uchaguzi huo Mohamed Farmajo baadhi ya vitu atakavyomiliki.

Kitu kilichobainika ni idadi ya zawadi kutoka kwa mataifa ya kigeni.

Image caption Rais wa zamani wa Somalia kushoto baada ya kumakabidhi rais mpya kulia mamlaka

Ikulu ya rais nchini humo imepokea zawadi kutoka kwa mashirika ya Umoja wa Ulaya hadi miungano ya vyuo vikuu vya Arabuni.