Mkenya atekwa nyara Msumbiji

Mji mkuu wa msumbiji Maputo
Image caption Mji mkuu wa msumbiji Maputo

Mkenya mmoja anayefanya kazi katika mtambo wa mahindi ametekwa nyara mjini Matola yapata kilomita 10 kusini magharibi mwa Mji mkuu wa Msumbiji Maputo.

Kisa hicho kulingana na mashahidi, kilitokea siku ya Alhamisi alfajiri yapata mita chache kutoka eneo la mtambo huo.

Maafisa wa polisi wanasema kuwa washukiwa hawajakamatwa.

Msemaji wa polisi Juarce Martins amenukuliwa akisema: Watekaji hao hawajawasiliana na ndugu, familia ama hata rafikize muathiriwa ambaye alikuwa mkurugenzi mkuu ili walipe kikombozi.Utekaji nyara kwa njia ya kupewa kikombozi umekuwa jambo la kawaida nchini Msumbiji.Awali waathiriwa walikuwa tajiri wenye asili ya bara Asia.