Waasi wa mwisho wa Colombia wajisalimisha

Wanachama wa Farc watasalimisha silaha zao ndani ya muda wa siku 180 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanachama wa Farc watasalimisha silaha zao ndani ya muda wa siku 180

Wanachama 300 wa mwisho wa kundi kuu zaidi la wapiganaji wa msituni nchini Colombia, FARC, wamewasili katika kambi ya kurekebisha tabia, ili wajumuishwe tena na raia.

Mwaka jana kundi la wapiganaji wa FARC, lilitia saini muafaka wa amani na serikali ya nchi hiyo, ili kumaliza uhasama wa mwagaji damu, uliodumu miongo kadhaa.

Takriban wapiganaji elfu 7 wameingia katika vituo zaidi ya 20, vya urekebishaji tabia na kukubalika katika jamii, baada ya kutembea mwendo mrefu kutoka maeneo ya milima milima na msituni, walikokuwa.

Image caption Wanachama wa FARC wakishauriwa na kamanda wao

Lakini Umoja wa mataifa, umeonyesha wasiwasi wake kuwa kambi hizo haziko tayari kuwapokea waasi hao.

Maafisa walikuwa wameomba serikali ya Colombia kuchelewesha kwa muda ratiba ya kusalimisha silaha, hadi pale silaha za kundi hilo la FARC, zimechukuliwa na kuhifadhiwa mahala salama, kwanza.

Image caption Ujenzi wa vituo vya kurekebisha tabia