Mugabe: Hakuna mtu anaweza kuchukua nafasi yangu

Rais Mugabe Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Mugabe

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amesema chama tawala cha ZANU-PF, pamoja na watu wa Zimbabwe hawaoni kama kuna mtu anaweza kuchukua nafasi yake katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Katika vyombo vya habari vya taifa, kabla ya kabla ya kutimiza miaka 93 hapo Jumanne, Rais Mugabe alisema watu wengi nchini Zimbabwe wengi hawaoni kama kuna mtu anayeweza kuchukua nafasi yake, ambaye anakubalika kama yeye.

Bwana Mugabe ameongoza nchi tangu mwaka wa 1980. Mwezi wa Disemba, ZANU-PF ilimthibitisha Mugabe kuwa mgombea wake katika uchaguzi ujao wa rais.