Trump amkaribisha mfuasi jukwaani Florida
Huwezi kusikiliza tena

Trump alivyomkaribisha mfuasi jukwaani Florida

Rais wa Marekani Donald Trump alimuita na kumkaribisha kwenye jukwaa, mmoja wa wafuasi wake, wakati wa mkutano wake wa hadhara katika jimbo la Florida.

Bw Trump alikuwa akihutubu alipomtambua mmoja wa wafuasi wake kwenye umati ambaye alisema alikuwa amemuona muda mfupi awali kwenye runinga.

Alimpa mfuasi huyo nafasi ya kuhutubia mkutano huo kutoka kwenye jukwaa lake.

Alieleza kwamba alifahamu walinzi wake wa Secret Service hawangefurahishwa na hatua hiyo yake, lakini akasema jambo pekee alilohofia kutoka kwa mfuasi huyo ni kwamba angeweza “kunipiga busu”.

Mada zinazohusiana