Wanandoa 160 watalakiana China ili kufaidika na fidia

Wanandoa nchini China.
Image caption Wanandoa nchini China.

Zaidi ya wanandoa 160 wanaoishi katika kijiji kimoja kusini mwa China wameama kutalakiana kwa lengo kupata kiwango kikubwa cha fidia itakayolipwa baada ya nyumba zao kuvunjwa kwa nguvu.

Kijiji hicho cha Jiangbei mashariki mwa China kinavunjwa ili kutoa nafasi ya ujenzi.

Wanandoa wanaoishi katika eneo hilo waligundua kwamba watafaidika na ujenzi wa nyumba mbili na takriban dola elfu 19 iwapo wataachana na kudai fidia hiyo wakiwa mbali mbali.

Baadhi ya wanandoa hao wana zaidi ya miaka 80, na wengi walisema walipanga kuendelea kuishi.