Vijana India sasa wanapata ushauri endelevu juu ya elimu ya jinsia

Wasichana wa shule ya Kashmiri katika mechi za Kriketi ya wanawake mjini Srinagar, tarehe 13 Septemba 2005. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Vijitabu vinaangazia masuala mbali mbali yanayofahamika kuwa mwiko kuzungumziwa nchini India

Vijitabu vya maelezo vya serikali ya India kwa ajili ya afya ya vijana walio katika umri wa kubarehe vimesifiwa kutokana na msimamo wake wa maelezo endelevu juu ya elimu ya jinsia

Vijitabu hivyo vya tume ya kitaifa ya afya nchini India , viliandikwa kwa ushikiano na mfuko wa Umoja wa Mataifa wa ongezeko la watu duniani, kwa lengo la "kuwawezesha vijana kutoa elimu kwa wenzao " - wasichana wadogo na wavulana ambao watakuwa na jukumu la kuwafikia vijana walio katika umri wa kubarehe na kujadiliana nao masuala yanayohusiana na ukuaji wao wa kimwili na kiakili.

Vijitabu hivyo vinaangazia masuala mbali mbali kuanzia unyanyasaji wa kingono, namna mtu anavyoweza kuvutiwa na mtu wa jinsia sawa na yake pamoja na afya ya akili, masuala ambayo huchukuliwa kama mwiko kujadiliwa na jamii za India.

Mpango wa vijana wanaotoa elimu kwa wenzao unatarajiwa kuendelea kote nchini India hivi karibuni.

Hizi ni baadhi ya agenda zinazoangaziwa kwenye vijitabu hivyo.

Kuvutiwa na mtu wa jinsia sawa na yako

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mapenzi ya jinsia moja ni mwiko nchini India

Vijitabu hivyo vinawaambia vijana walio katika umri wa kubarehe wanaojitolea kwamba : "Ndio, vijana walio katika umri wa kubarehe mara kwa marahujipata katika mapenzi . Wanaweza kuhisi wanampenda mtu ama rafikiama mtu wa jinsia tofauti ama hata wa jinsia sawa na yao. Ni jambo asilia na la kawaida kuwa na hisia za kipekee kwa mtu fulani."

Hili ni kinyume na hali ya kisheria kwa wapenzi wa jinsia moja nchini India. Mahusiano ya kimapenzi ya watu wa jinsia moja ni kosa la jinai katika nchi nchi hiyo na mwenye kupatikana huadhibiwa kwa kifungo cha miaka 10 hadi cha maisha jela . Pia mapnzi ya jinsia moja huchukuliwa kama kitu ambacho ''si cha kawaida'' na wapenzi wa jinsia moja mara kwa mara hukabiliwa na unyanyapaa miongoni mwa jamii zao.

"Vijana walio katika umri wa kubarehe mara kwa mara hujihisi kama watu wasio na haki katika mahusiano yao ya kimapenzi. Ni wakati wa mabadiliko makubwa kwao na juhudi zozote zinazojaribu kuwasaidia kukabiliana na mambo haya ni kitu kizuri ," Dk. Samir Parikh, mshaui wa masuala ya kisaikolojia kwa vijana wanaobarehe , aliiambia BBC.

"Kwa sasa, kuna ukwepaji wa elimu hii inapokuja katika namna ya kukabiliana na masuala ya aina hii miongoni mwa vijana. Kile kinacholifanya suala hili kuwa la dharura zaidi ni kwamba tayari vijana wana taarifa zisizo kamili na zenye kupotoshwa kutokana na ukweli kwamba Intaneti na habari kwa ujumla zimefika kila kona ya nchi ."

Mzunguko wa hedhi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanawake na wasichana wenye hedhi hawaruhusiwi kufika kwenye maeneo mengi ya dini ya kuabudu

Mwanamke mwenye hedhi huaminiwa na wengi nchini India kama "asiye msafi " . Wanawake wenye hedhi hawaruhusiwi kuingia katika maeneo mengi ya ibada za kidini , na wakati mwingine hawaruhusiwi hata kuingia jikoni katika nyumba zao.

Vijitabu vya maelezo vinajaribu kueleza ni nini maana ya hedhi ,na kuelezea kwamba "Msichana aliye katika umri wa kubarehe hapaswi kuhisi aibu ama mwenye makosa kwa kuwa na hedhi, wanapaswa kuendelea na shughuli zao za kila siku na kula chakula chenye virutubisho na kuwa wasafi zaidi katika siku hizi ".

VInaongeza kuwa "Hedhi si 'chafu' ama kitu 'kinachochafua mazingira'. Kama usafi utazingatiwa wasichana wanaweza kuendelea na shughuli zao za kawaida ikiwa ni pamoja na masomo, michezo, mapishi, na kufanya kazi nyingine zozote zile kwa faraja na heshma ."

Wavulana wanaweza kulia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wavulana katika umri mdogo huambiwa kuwa hawapaswi kulia ama kuonyesha hisia zao

Dhana kuhusu jinsia ya kiume pia imeangaziwa katika vijikaratasi vya maelezo juu ya elimu ya jinsia.

Katika jamii inayotawaliwa na mfumo dume , wavulana hawaruhusiwi kuonyesha hisia za ulegevu na wanaambiwa katika umri mdogo kwamba hawapaswi kulia ama kuonyesha hisia zao.

Ubaguzi wa kijinsia unawaweka wanaume katika majukumu ambayo yanaonekana na jamii kuwa ya watu shupavu na kuwaambia wasichana kuwa wanapaswa kuongea kwa utaratibu na kama wanawake .

Vijitabu hivyo vinasema ni SAWA kwa mvulana ama mwanamume kulia kuonyesha hisia zake , kuongea kwa upole ama kuwa mwenye aibu na ni SAWA kwa msichana kuzungumza wazi ama kuvalia nguo kama za mvulana na kucheza michezo kwa ujumla inayotambuliwa kama michezo ya wavulana.

Kuwahimiza wasichana kucheza michezo ya viwanjani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption mara nyingi wasichana wanatarajiwa kubaki majjumbani mwao na kusaidia kazi za nyumbani

Wazazi wengi wa India hawawaruhusu wasichana kushiriki michezo ama kucheza nje ya nyumba zao kabla ya kufikia umri wa kubarehe.

Wakati huu, mara kwa mara wanatarajiwa kuwa majumbani na kusaidia kazi za nyumbani. Hii inatokana na sababu mbali mbali ikiwemo usalama, hofu kwamba wakiwa karibu na wavulana wanaweza kujipata katika uhusiano '' usiofaa'' na pia dhana kwamba msichana "ni mtu ambaye haogopi".

Vijitabu hivyo vinazungumzoa juu ya umuhimu wa mazoezi ya mwili kwa wasichana na wavulana na katika sehemu inayowahusu wavulana inasema : " Kama watu wenye wajibu katika jamii , tunapaswa kuhakikisha kwamba wasichana hawaambiwi maneno ya kebehi ama kunyanyaswa kimwili na kimaneno ."

Maelezo hayo yanaendelea kusema kuwa kutowaruhusu wasichana kushiriki michezo na shughuli nyingine nje ya majumbani mwao "si vema kwa afya yao ya mwili, na huwafanya wasijiamini na kuweza kuchukua maamuzi yao wenyewe ".