Barca, Real Madrid zapeta la liga

La liga Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wachezaji wa Barcelona wakipongezana baada ya Messi kufunga

Miamba ya soka ya nchini Hispania, Barcelona na Real Madrid wameendelea na wimbi la ushindi katika michezo ya kuwania ubingwa wa la liga.

Barcelona wakicheza katika uwanja wao wa Nou Camp wamewachapa Sevilla kwa mabao 3-0, magoli ya Barca yakifunga na Luis Suarez na lionel Messi aliyefunga mara mbili.

Real Madrid wakiwa ugenini wameshinda kwa mabao 4-2 dhidi ya Leganes,Mshambuliaji Alvaro Morata akifunga hattrick na bao jingine likifungwa na James Rodriguez, mabao ya Leganes yakifungwa Gabriel Pires,na Luciano Neves.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji wa Real Madrid James Rodriguez akikabwa na beki wa Leganes Tito

Alaves wakalala nyumbani kwa bao 1-0 dhidi ya Osasuna, Deportivo La Coruna wakatoshana nguvu na Granada kwa sare ya bila kufungana , Malaga wakawatambia Sporting Gijon nyumbani kwa kuwafunga bao 1-0.