Mafuriko yasababisha mji wote kuhamwa New Zealand

Mafuriko yasababisha mji wote kuhamwa New Zealand Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mafuriko yasababisha mji wote kuhamwa New Zealand

Mji wote wa Edgecumbe ulio kisiwa cha Kaskazini mwa New Zealand, umehamwa baada ya mafuriko makubwa.

Takriban nyumba 600 na watu 200 wameathiriwa na sasa mashua zinatumiwa kuwaokoa watu.

Mvua iliyosababishwa na kimbunga Debbie ambacho kilikumba Australia wiki moja iliyopita, imasababsiha mito kuvunja kingo zake.

Watabiri wa hali ya hewa wanaitaja hali iliyokumba nchi hizo mbili kuwa inayotokea mara moja katika miaka 500.

Mawimbi makali pia yanashuhudiwa katika kisiwa kilicho kusini mwa New Zeakand.

Katika mji wa Edgecumbe maji yanasemekana kufika hadi mita 2 katika baadhi ya maeneo.

Polisi wanasema watapiga doria katika maeneo yaliyohamwa na kuweka vizuizi kuwazuia raia wasije wakarudi.

Haki miliki ya picha TVNZ
Image caption Mafuriko yasababisha mji wote kuhamwa New Zealand
Image caption Mafuriko yasababisha mji wote kuhamwa New Zealand
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mafuriko yasababisha mji wote kuhamwa New Zealand

K