Liverpool kumkosa Sadio Mane mechi zilizosalia

Sadio Mane baad ya kupata jerha la goti katika mechi dhidi ya Everton
Image caption Sadio Mane baad ya kupata jerha la goti katika mechi dhidi ya Everton

Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane huenda asishiriki mechi saba za lig zilizosalia msimu huu kutokana na jeraha la goti.

Mane mwenye umri wa miaka 24 alitolewa uwanjani baada ya kugongana na Leighton Banes katika mechi ya ushindi wa 3-1 ya siku ya Jumamosi dhidi ya Everton.

Meneja Jurgen Klopp alisema kuwa ana hakika Mane alihitaji kufanyiwa upasuaji , hatua inayomfanya kuwa vigumu kushiriki katika mechi yoyote msimu huu.

Mchezaji huyo kutoka Southampton aliyesajili kwa kitita cha pauni milioni 34 ameanzishwa mechi zote isipokuwa tano pekee za Liverpool msimu huu.

Kati ya mechi hizo tatu zilipata matkeo ya sare huku mbili zikipotezwa.

Liverpool iko katika nafasi ya tatu katika jedwali la ligi huku ikiwa zimesalia mechi saba.