Chama cha UDP chashinda viti vingi bungeni Gambia

Matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa bunge wa Gambia uliofanywa Alhamisi umoenyesha kuwa chama cha United Democratic Party kimeshinda. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa bunge wa Gambia uliofanywa Alhamisi umoenyesha kuwa chama cha United Democratic Party kimeshinda.

Matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa bunge wa Gambia uliofanywa Alhamisi umoenyesha kuwa chama cha United Democratic Party kimeshinda.

Chama hicho kilishinda viti 31 kati ya viti 58 ambapo kilikishinda pakubwa chama cha APRC - chama kilichokuwa na Wabunge wengi, chini ya utawala wa mbabe aliyetimuliwa, Yahya Jammeh, ambacho kwa wakati huu kilipata viti vitano pekee.

Kiongozi wa UDP, Ousaiho Darbboe, alisema kuwa yeye anaunga mkono kiongozi wa sasa, Adama Barro.

Ni asilimia 42 ya wapiga kura waliojitokeza, wachanganuzi wakisema raia wengi wa Gambia wamechoshwa na siasa baada ya kutengwa kwa muda mrefu na Rais Yahya Jammeh.