Mke na mumewe kutoka Kenya washinda mbio za Paris Marathon

Paul Lonyangata akiibuka mshindi katika mbio za Paris Marathon Haki miliki ya picha AFP
Image caption Paul Lonyangata akiibuka mshindi katika mbio za Paris Marathon

Mkenya Paul Lonyangata alipata ushindi mkubwa wa saa 2 dakika 6 na sekunde 10 katika historia yake licha ya kupoteza muda bora.

Mpinzani wake pia kutoka Kenya katika mbio hizo Stephen Chebogut alikuwa wa pili kwa muda wa saa 2 dakika 6 na sekunde 56 huku Solomon Yego pia wa Kenya akishikilia nafasi ya tatu katika muda wa saa 2 dakika 7 na sekunde 13.

''Nahisi vyema sasa kwa sababu lengo langu lilikuwa kuja hapa na kuibuka mshindi '',alisema.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Mtu na mkewe kutoka Kenya washinda mbio za Paris Marathon

Huku Paris ikiwa na jua Rionoripo ambaye ni mkewe mshindi wa mbio hizo upande wa wanaume Paul Lonyangata aliibuka mshindi.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 23 aliweka muda bora wa saa 2 dakika 20 na sekunde 50 na hivyobasi kushinda muda wake binafsi aliouweka kwa zaidi ya dakika 4.

Ushindi wa wanandoa hao ulirudisha tabasamu kwa wanariadha Wakenya baada ya habari za kushangaza kwamba bingwa wa mbio za marathon za Olimpiki upande wa wanawake Jemima Sumgong alipatikana ametumia dawa za kusisimua misuli.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mkewe Lonyangata akivuka utepe kushinda mbio za Paris marathon upande wa wanawake

Sumgong ni Mkenya wa kwanza mwanamke kushinda medali ya Olimpiki katika mbio za marathon alipoibuka mshindi katika michezo ya Olimpiki ya Rio.

Mwanariadha huyo ambaye pia ni bingwa mtetezi wa mbio za london Marathon alipatikana alitumia dawa aina ya EPO baada ya kufanyiwa uchunguzi na IAAF.

Lonyangata mwenye umri wa miaka 24 aliamua kuongeza kasi baada ya kilomita 35 akampita Chebogut na hivyobasi kujiongezea mataji aliyoshinda katika mbio za Shanghai marathon 2015 pamoja na Lisbon miaka miwili mapema.

Katika mbio za wanawake Rionoripo alifuatwa kwa karibu na Mkenya mwenzake Agnes Barsosio kwa kuweka muda wa saa 2 dakika 21 na sekunde 02 huku Flomena Cheyech akimaliza udhia.

Rionoripo alivunja rekodi iliokuwa imewekwa na raia wa Ethiopia Feyse Tadese ya saa 2 dakika 21 na sekunde 06 mwaka 2013