Maandamano yaningia siku ya pili Venezuela

Waandamanaji wakabiliana na Polisi Venezuela
Image caption Waandamanaji wakabiliana na Polisi Venezuela

Polisi katika mji mkuu wa Venezuela, Caracas,wameendela kutumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kuwazuaia waandamanaji waliongia siku wakipinga serikali ya Rais Nicolas Maduro.

Wanaharakati walioficha nyuso zao wamewarushia polisi mawe na mabomu yaliyotengenezwa kwa petrol.

Vurugu hizo zinaendelea katika maeneo ya mashariki mwa mji wa Caracas,ambako ndiyo ngome kuu ya upinzani.

Siku ya jumatano watu watatu walikufa katika maandamano mjini Caracas na magharibi mwa Venezuela. Wapinzani wanakasirishwa na kuzorota kwa hali ya uchumi,ambapo wanahitaji uchaguzi mkuu kufanyika.