Picha bora zaidi Afrika: 13-20 Aprili.

Baadhi ya picha zilizovutia kutoka nchi tofauti barani Afrika na za Waafrika walioko maeneo mbali mbali duniani wiki hii.

Waimbaji wa nyimbo za injili wakiwa wamevalia nguo za utamaduni wakati wa ibada mjini Johannesburg, Afrika Kusini. EPA/Picha - 14 Aprili 2017 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Waimbaji wa nyimbo za injili wakiwa wamevalia nguo za utamaduni siku ya Ijumaa njema wakati wa ibada mjini Johannesburg, Afrika Kusini...
Wakristo wanabeba msalaba wakati wa maandamano yasiyokuwa na kelele, mjini Durban, Afrika Kusini. Aprili 14, 2017. REUTERS/Rogan Ward Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Huku Wakristo hawa wakibeba msalaba wakati wa maandamano yasiyokuwa na kelele, Afrika Kusini..
kuhani wa kanisa la Orthodox wakati wa maombi ya usiku wa kuamkia Pasaka mjini Addis Ababa, Ethiopia, Aprili 15, 2017. Picha ya REUTERS/Tiksa Negeri Haki miliki ya picha Photoshot
Image caption Siku iliyofuata, kuhani wa kanisa la Orthodox nchini Ethiopia awabariki wafuasi mjini Addis Ababa.
Msichana kutoka Sudan aonyesha uso wake uliochanjwa siku ya Jumapili katika soko lililopo kilomita 480 kutoka mji mkuu Khartoum. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Msichana kutoka Sudan aonyesha uso wake uliochanjwa siku ya Jumapili katika soko lililopo kilomita 480 kutoka mji mkuu Khartoum.
Washiriki wa gwaride la heshima nchini Zimbabwe katika sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya uhuru siku ya Jumanne. Picha ya AFP / 18 Aprili 2017 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Washiriki wa gwaride la heshima nchini Zimbabwe siku ya Jumanne katika sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya uhuru kutoka Uingereza.
Waziri wa Usalama Marekani James Mattis aondoka baada ya kuweka shada la mau wakati wa ukumbusho wa askari asiyejulikana mjini Cairo Aprili 20, 2017. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Makumbusho ya "Askari Asiyejulikana" katika mji mkuu Misri, Cairo yalipigwa picha Alhamisi wakati wa ziara ya Waziri wa Usalama Marekani James Mattis
Bunge la Morocco wakati wa mkutano wa pamoja wa umma mjini Rabat, mnamo Aprili 19, 2017, / Picha ya AFP Haki miliki ya picha AFP
Image caption Siku hiyo hiyo, katika mji mkuu wa Morocco, Rabat, mbunge mwanamke anapigwa picha akivuka sakafuni katika mkutano wa pamoja bungeni.
Paa akinywa maji kutoka bwawa katika hifadhi ya taifa Dinder, katika eneo la Sennar nchini Sudan./ Picha ya AFP 14 Aprili Haki miliki ya picha AFP
Image caption Picha hii iliopigwa Ijumaa yaonyesha paa kando ya bwawa la maji katika hifadhi ya taifa nchini Sudan.
Wapiganaji wa kike na watoto wao waketi katika ukumbi wa kituo cha ukarabati jijini Mitiga, Tripoli nchini Libya. Aprili 19, 2017. REUTERS/Ismail Zitouny Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Siku moja kabla, wapiganaji wa kike kutoka makundi ya wapiganaji wa Kiislamu wanaketi katika kituo cha ukarabati katika mji mkuu Libya, Tripoli.
Mvulana kutoka Tunisia auza nguo katika soko katikati mwa jiji la Tunis, Aprili 14, 2017. Picha ya AFP / FETHI BELAIDFETHI Haki miliki ya picha AFP
Image caption Katika nchi jirani ya Tunisia, ambapo maafisa walianzisha mradi dhidi ya kuajiri watoto, mvulana mmoja siku ya Ijumaa anauza nguo katika soko katika mji mkuu Tunis.

Images courtesy of AFP, EPA, Getty Images and Reuters

Mada zinazohusiana