Kwa Picha: Nyanya wa miaka 85 aliyetimiza ndoto ya kuwa msanii

Haki miliki ya picha JASMEEN PATHEJA
Image caption Kutokana na ushirikiano wao walianzisha mradi unaojulikana kama "Indri and I"

Msanii mmoja nchini India ambaye pia mwanaharakati Jasmeen Patheja wakati wote alikuwa na ndoto ya kuwa mpiga picha.

Na miaka kadha iliyopita, wakati nyanya yake Inderjit Kaur alisema alikuwa ndoto ya kuwa mcheza filamu, wawili hao waliamua kutimiza ndoto zao.

Kutokana na ushirikiano kati yao walianzisha mradi unaojulikana kama "Indri and I" mzururu wa picha unaomuonyesha nyanya huyo wa umri wa miaka 85 akiwa amevalia mavazi ya kupendeza.

Haki miliki ya picha JASMEEN PATHEJA
Image caption Anakumbuka nyakati za majira ya joto akiwa mtoto alipokuwa akiishi mji ulio mashariki mwa India wa Kolkata akirudi nyumbani kutoka shuleni.

"Sitasema haswa tarehe mradi huu ulianza. Huenda ulianza nikiwa na umri wa miaka mitatu," Bi Patheja aliiambia BBC.

Anakumbuka nyakati za majira ya joto akiwa mtoto alipokuwa akiishi mji ulio mashariki mwa India wa Kolkata akirudi nyumbani kutoka shuleni.

Haki miliki ya picha JASMEEN PATHEJA
Image caption Bi Kaur alikuwa mke wa nyumbani na masomo yake yalitatizwa na sintofahamu ya Vita vya Pili vya Dunia

Bi Kaur alikuwa mke wa nyumbani na masomo yake yalitatizwa na sintofahamu ya Vita vya Pili vya Dunia. Mzaliwa wa Burma ambayo sasa ni Mynmar, alitoroka na familia yake kuenda Lahore katika iliyo sasa Pakistan akiwa na umri wa miaka 9 wakati Japan iliishambulia India.

"Wakati mwingine anaweza kusemea, "Laiti ningesoma zaidi." anajutia fursa iliyopotea ya kutosoma.

Haki miliki ya picha JASMEEN PATHEJA
Image caption Pia alifurajia kupigwa picha na alikuwa mtu wa kawaida tu mbele ya kamera

Pia alifurajia kupigwa picha na alikuwa mtu wa kawaida tu mbele ya kamera, Bi Patheja anasema.

"Kwa hivyo miaka michache iliyopita, siku moja alisema, nahisi ningekuwa mcheza filamu, ndipo nikase sawa, "hucheze nami nichukue picha," Ndivyo alizaliwa "Mcheza filamu Indri."

Haki miliki ya picha JASMEEN PATHEJA
Image caption Pia alifurajia kupigwa picha na alikuwa mtu wa kawaida tu mbele ya kamera

Wote walianza kupiga picha tofauti ambazo Indri alikuwa na ndoto kuzihusu.

Haki miliki ya picha JASMEEN PATHEJA
Image caption Kwa miaka kadha alishuhudia nyanya huyo akiigiza kama mwanasayasni, malkia, mwanasayansi na mambo mengine kadha.

Kwa miaka kadha alishuhudia nyanya huyo akiigiza kama mwanasayasni, malkia, mwanasayansi na mambo mengine kadha.

Haki miliki ya picha JASMEEN PATHEJA
Image caption Picha hizo wakati mwingine huonyesha uhusiano ulio kati ya nyaya na mjukuu

Picha hizo wakati mwingine huonyesha uhusiano ulio kati ya nyaya na mjukuu, wanawake wawili ambao walikuwa wakitaka kusaidiana maishani.

Haki miliki ya picha JASMEEN PATHEJA
Image caption Tangu picha hizi zichapishwe wanawake wengi hasa wale wazee, wameaniandika wakipongeza mradi huu

Tangu nichapishe picha hizi mapema Aprili wanawake wengi hasa wale wazee, wameaniandikia wakipongeza mradi huu. Pia umesifiwa na wanawake walio karibu na nyanya zao au wajukuu.