Mwanasiasa wa Ethiopia Yonatan Tesfaye afungwa kwa sababu ya ujumbe Facebook

Yonatan Tesfaye Haki miliki ya picha Yonatan Tesfaye
Image caption Yonatan Tesfaye amefungwa jela miaka 20

Mwanasiasa wa upinzani Ethiopia Yonatan Tesfaye amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 6 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kuendekeza ugaidi kwa ujumbe aliyouandika katika mtandao wa kijamii Facebook, limeripoti gazeti la Addis Standard.

Linaongeza kuwa mahakama imekubali ombi lake la kumhukumu kifungo cha chini zaidi.

Mapema mwezi huu shirika la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International lilitaja hatua hiyo ya kumpata na hatia kama "uavyaji wa sheria".

Alikamatwa Desemba 2015 wakati maandamano ya kuipinga serikai katika eneo la Oromia yalipochacha.

Maafisa wa utawala wamepinga maandishi kadhaa aliyoweka ikiwemo kauli aliyotoa ambapo alisema serikali ilitumia "nguvu dhidi ya watu badala ya kufanya majadiliano ya amani".

Ethiopia imeshutumia kwa kutumia sheria za kupambana na ugaidi kunyamazisha wapinzani.

Amnesty International walisema madai hayo dhidi yake ni ya kusingiziwa yalipothibitishwa Mei 2016.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waandamanaji kutoka Oromia na Amhara wamekuwa wakilalamikia kutengwa kisiasa na kiuchumi

Watu zaidi ya 600 walifariki dunia wakati wa makabiliano kati ya maafisa wa usalama na waandamanaji, kwa mujibu wa shirika la haki za kibinadamu la serikali.

Serikali ilianza kutekeleza sheria ya hali ya hatari Oktoba mwaka jana ili kudhibiti hali.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii