Wizi wa mitungi ya oksijeni Everest wazua wasiwasi

Wakwea milima huhitaji mitungi ya gesi ya oksijeni kufika kilele cha mlima Everest Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Wakwea milima huhitaji mitungi ya gesi ya oksijeni kufika kilele cha mlima Everest

Wakwea milima kutoka nchi za nje pamoja na wasaidizi ambao hufahamika sana kama Sherpa katika Mlima Everest, wameeleza wasiwasi wao kutokana na kukithiri kwa wizi wa mitungi ya oksijeni katika kambi zilizo maeneo ya juu katika mlima huo.

Wamesema hilo huenda likahatarisha maisha ya watu wanaopanda milima hiyo kwa sababu kila mtu hubeba gesi ya kumtosha yeye pekee.

Wameibua hilo huku makundi ya mwisho ya wakwea milima wakisubiri hali ya hewa iwe nzuri kabla ya kujaribu kufika kileleni.

Wataalamu wanasema umati wa wakwea milima, wengi ambao hawana ujuzi wowote na waelekezi na wasaidizi wao pia hawana ujuzi, wamechangia kukithiri kwa tatizo katika kuukwea mlima huo mrefu zaidi duniani.

"Linakuwa tatizo kubwa sana sasa huko juu," Nima Tenji Sherpa, mwelekezi wa wapanda milima ambaye amerejea kutoka Evereset ameambia BBC.

"Nilikuwa nikisikia mara kwa mara kutoka kwa makundi ya wakwea milima kwamba mitungi ya gesi ilikuwa imetoweka na kwamba kuna watu ambao maisha yao huenda yalikuwa hatarini - hasa wakati wamemaliza gesi waliyokuwa wamebeba na bado hawajafika kileleni, au wanapaka kutumia mitungi ambao imehifadhiwa kambini wanapokuwa wanarejea chini."

Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Wakwea milima hulipa $11,000 kupata leseni ya kuukwea Mlima Everest

Baadhi ya wapanda milima wamekuwa wakiandika kwenye Facebook kuhusu kuibiwa kwa mitungi yao ya gesi.

"Mitungi mingine saba ya oksijeni imeibiwa kutoka kwa hazina yetu," aliandika kiongozi wa kundi moja Tim Mosedale katika Facebook Jumatatu iliyopita.

"Wakati huu ni South Col (kambi ya nne, kambi ya mwisho kabla ya kufika kileleni Mlima Everest ambayo inapatikana 7,900m)."

Visa vya watu kufariki kutokana na ukosefu wa oksijeni huripotiwa mara kwa mara.

Mwaka huu, kulikuwa kumeripotiwa vifo vya wapanda milima 10, lakini maafisa wa Nepal wanasema vifo vilivyothibitishwa ni vya watu watano pekee kufikia sasa.

Hata hivyo, hakuna aliyedaiwa kufariki kutokana na wizi wa mitungi ya oksijeni.

Haki miliki ya picha DEVENDRA M SINGH
Image caption Mpanda milima kutoka Japan akiwa na mitungi isiyo na oksijeni Kathmandu

Nima Tenji Sherpa anasema wakati mmoja, alilazimika kumpa mteja wake mtungi wake wa oksijeni mwaka 2012 walipokuwa wanarejea baada ya kugundua kwamba mitungi waliyokuwa wameacha kambili ilikuwa imeibiwa.

"Ni baharti kwamba tuliweza kufika katika kambi za chini."

Wakwea milima sana hutumia mitungi ya oksijeni wakipanda baada ya kuondoka Kambi ya Tatu.

Kufikia sasa, Masherpa wanasema hakuna aliyenaswa akiiba mitungi ya gesi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii