Shambulizi la Manchester lilipangwa tokea Desemba

Salman Abedi na gari lake kulia wakati akijiandaa kwa shambulizi hilo
Image caption Salman Abedi na gari lake kulia wakati akijiandaa kwa shambulizi hilo

Maafisa usalama wa serikali inayoungwa mkono na umoja wa Mataifa nchini Libya imeiambia BBC kuwa shambulizi la mjini Manchester lilipangwa tokea mwezi Desemba.

Wanasema kuwa mshambuliaji Salman Abedi, alikua akifuatiliwa nyendo zake na wanausalama wa Libya kabla ya kusafiri kuelekea Uingereza kufanya shambulizi hilo.

Image caption Watu 22 waliuawa na wengine 59 kujeruhiwa

Mmoja wa kaka yake (Hashem) na baba yake (ramadan) pia walikuwa wakifuatiliwa na kwa sasa wanashikiliwa na polisi.

Haijawekwa wazi iwapo maafisa wa Libya walitoa taarifa kwa wale wa Uingereza.