Gavana wa zamani afungwa miaka 14 Brazil

Sergio Cabral alihusika kwa kiasi kikubwa kwenye ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya michuano ya Olimpiki
Image caption Sergio Cabral alihusika kwa kiasi kikubwa kwenye ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya michuano ya Olimpiki

Mahakama nchini Brazil imemuhukumu gavana wa zamani wa jimbo la Rio de Janeiro Sergio Cabral, miaka 14 gerezani kwa kuhusika katika rushwa na utakatishaji wa fedha.

Cabral anatajwa kuhusika kwenye upokeaji wa mamilioni ya dola katika miaka nane aliyokuwa madarakani.

Fedha hizo ni sambamba na zile za makampuni yaliyopata mkataba wa kujenga miundombinu wakati wa michuano ya Olimpiki.

Image caption Jaji aliyetoa hukumu hiyo Sergio Moro anasema hakuna aliyeonewa wala kupendelewa

Jaji Sergio Moro ambaye ndiye aliyetoa hukumu hiyo amesema hakuna ushahidi wa kutosha kama mke wa Cabral aitwaye Adriana Ancelmo ambaye pia ni mwanasheria maarufu nchini humo alihusika.