Israel yashambulia ngome ya majeshi ya Syria kwa siku ya pili

Hii ni siku ya pili mfululizo kwa mashambulizi hayo
Image caption Hii ni siku ya pili mfululizo kwa mashambulizi hayo

Israel imeshambulia ngome ya majeshi ya serikali ya Syria kwa siku ya pili, baada ya kombora la wanajeshi hao kuanguka kwa bahati mbaya katika eneo la Golan linaloshikiIiwa na Israel kusini magharibi mwa taifa hilo.

Israel mara kwa mara imekuwa ikifanya mashambulizi ya angani na kujibu mashambulizi wakati wa mzozo wa Syria lakini imejizuia kuhusika na mzozo huo moja kwa moja.

Iliteka eneo la Golan kutoka kwa Syria wakati wa mapigano ya mwaka 1967.