Maafisa wa Urusi na Marekani wakutana

Majengo ya Urusi yanayoshikiliwa na Marekani Haki miliki ya picha AFP
Image caption Majengo ya Urusi yanayoshikiliwa na Marekani

Mazungumzo kati ya maafisa waandamizi wa Marekani na Urusi yamemalizika mjini Washington juu ya madai ya Moscow kutaka kurudishiwa majengo yake mawili wanayofanyia shughuli za kibalozi yaliyokuwa yakishikiliwa toka Desemba mwaka jana na utawala wa Rais aliyemaliza muda wake Barack Obama.

Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kwa Waandishi wa Habari, lakini alipoulizwa na Wanahabari waliokuwa wakisubiri kujua hatma ya mazungumzo yao, maafisa wa Urusi walijibu kwa kifupi kwa kusema ''..takriban yote yamefikiwa..''.

Awali Urusi ilionya kuchukua hatua ya kulipiza kisasi iwapo vifaa katika majengo hayo vinawekwa tena. maeneo hayo yaliyokuwa yakishikiliwa na Marekani kutokana na madai kuwa yalikuwa yakitumiwa kwa shughuli za kiitelejensia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov ameishutumu Marekani kwa kile alichokiita ''..Wizi wa wazi''

Hali ya kisiasa nchini Marekani imekuwa mbaya katika wakati pia uchunguzi juu ya Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Rais nchini humo ukiendelea