Rais Trump na Putin walikutana kisiri

Rais wa Marekani na mwenziye wa Urusi
Image caption Rais wa Marekani na mwenziye wa Urusi

Ikulu ya Marekani imethibitisha kuwa Rais Donald Trump alifanya mazungumzo zaidi ambayo awali hayakuelezwa na Rais Vladmir Putin wa Urusi wakati wa mkutano wa viongozi wa nchi zilizoendelea Kiuchumi G20, mapema mwezi huu nchini Ujerumani.

Imeuelezea mkutano huo kama ''..Mazungumzo mafupi..'' ambayo yalifanyika saa kadhaa baada ya mazungumzo rasmi ya pande mbili kati ya viongozi hao wawili.

Baadhi ya Taarifa zinadokeza kuwa Rais Trump alizungumza na Rais Putin kwa takriban saa baada ya kupata mlo wa jioni.

Ikitoa ufafanuzi zaidi, Ikulu ya Marekani imesema mkalimani wa lugha ya Kirusi alikuwepo wakati wakati aliyekuwepo wa Marekani alikuwa hazungumzi lugha ya Kirusi.

Hata hivyo kilichozungumzwa na viongozi hao wawili bado hakijawekwa wazi.

Taarifa hizo zinakuja wakati ambao uchunguzi mjini Washington ukiendelea juu ya uwezekano wa kufanyika makubaliano ya siri kati ya timu ya Rais Trump na Moscow wakati wa kampeni za Urais, katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mwaka 2016.